Thursday, 23 April 2015

JORDAN HENDERSON ATIA SAINI MKATABA

           
Kiungo wa Liverpool Jordan Henderson amesaini mkataba mpya na klabu yake wa miaka mitano wenye thamani ya pauni 100,000 kwa wiki.
Mkataba huu mpya utamuweka kiungo huyu klabuni hapo mpaka mwaka 2020
Henderson alisajiliwa na majongoo wa Anfield mwaka 2011 kwa kiasi cha pauni 20 millioni akitokea katika klabu ya Sunderland.
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amesisitiza wamiliki watimu hiyo wanataka kujenga imara itakayokua pamoja na kutwaa vikombe.
Wakati nahodha wa sasa Steve Gerrard akiwa anaondoka mwishoni mwa msimu na kuelekea katika timu ya LA Galaxy ya Marekani , Henderson ndio anaoneka kama mbadala wa sahihi wa gerrard.

No comments:

Post a Comment