Klabu za Bayern Munich ya Ujerumani
na Barcelona ya Hispania zimetinga nusu Fainali katika ligi ya Mabingwa
barani Ulaya baada ya kushinda mechi zao hapo jana usiku.
Nao Barcelona baada ya ushindi wa awali wa bao 3-1 dhidi ya Paris st Germen, mjini Paris ,hapo jana imeendeleza vipigo dhidi ya Wafaransa hao baada ya kuwakandamiza bao 2-0,zilizowekwa kimiani na Mbrazil Neymar katika kipindi cha kwanza.Kwa matokeo hayo Barcelona imefuzu nusu fainali kwa ushindi wa jumla ya magoli 5-1.
Mechi nyingine za robo fainali zinakamilika hii leo , pale Juventus ya Utaliano itakaposhuka dimbani kuwakabili Monaco ua Ufaransa,huku shughuli nyingine pevu ikitarajiwa kuonekana kwenye dimba la Santiago , pale mabingwa watetezi Real Madrid watakapo wakaribisha mahasimu wao Atletico Madrid.
No comments:
Post a Comment