Monday, 27 April 2015

HAYA SASA ... YA MZEE MAJUTO NA HARAKATI ZA KUOA MJUKUU WAKE ... !!

Vunja ukimya! Komediani namba moja Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ amegeuka mbogo baada kuulizwa juu ya madai ya kuoa binti mdogo ambaye ni sawa na mjukuu wake mwenye umri wa miaka 18 akidai kuwa sheria ya dini inamruhusu kufunga ndoa wa wake wanne.

              Komediani namba moja Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda ambalo ndilo lililokuwa la kwanza kuripoti ishu hiyo, Mzee Majuto ambaye awali alionesha kuwa na jazba alifunguka:
“Hilo suala haliwahusu wala na si jambo la ajabu kabisa kwa sababu mimi ni mwanaume wa Kiislamu, sheria ya dini inaniruhusu kuoa mke wa kwanza wa pili wa tatu hadi wanne,” alisema Majuto

No comments:

Post a Comment