MUSA MATEJA NA IMELDA MTEMA
Hatimaye lile sekeseke la ndoa ya meneja wa wasanii wa Bongo Fleva
wanaosimamiwa na Kampuni ya Endless Fame, Petit Man na mdogo wa
mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Platnumz limemdondokea
Wema Isaac Sepetu anayedaiwa kuitibua kiasi cha kuwatenganisha na kila
mmoja kuchukua hamsini zake.
Habari kutoka chanzo chetu zilidai kwamba, Wema amehusika kwa
asilimia kubwa kutibua ndoa hiyo kwani amekuwa akimtafutia mademu Petit
Man, jambo ambalo Esma alilishtukia na kuamua kumbwatukia Wema kwa
kuandika maneno makali kwenye mitandao ya kijamii.
“Kwa taarifa yenu Esma anamlalamikia Wema kuwa anamfanya mumewe kuwa
mhuni kiasi kwamba anachukua mademu, tena marafiki zake na hata
akimuuliza Petit Man anajifanya hao ni mashoga wa Wema.“Anapomkomalia,
mara kadhaa umekuwa ukizuka ugomvi mkubwa na Petit Man anahama nyumbani
kwake na kukimbilia kwa Wema,” kilisema chanzo chetu.Baada ya
kunyetishiwa ‘infomesheni’ hizo, gazeti hili liliingia kazini kusaka
ukweli wa mambo yanayodaiwa.
Lilianzia kwa Esma, alipopatikana alisema ni kweli hivi karibuni
aliandika ujumbe kwenye Mtandao wa Instagram, ingawa kwenye maelezo yake
hakumtaja mtu bali aliandika kwa hisia kama binadamu mwingine
anavyoweza kuandika.
“Nani anasema nimemtukana mtu? Niliandika mambo ambayo nilijisikia
mwenyewe lakini sikumtaja wala kumlenga mtu yeyote, kama kuna mtu
alikwazika basi atakuwa anajichanganya mwenyewe.“Mimi sina tatizo na
Wema na mambo ya familia yangu siwezi kumwambia kila mtu hivyo kama kuna
ugomvi kati yangu na mume wangu hayo ni mambo ya familia yetu,” alisema
Esma.
Kwa upande wake Wema alifunguka kwamba hajawahi kuongea jambo na Esma
na kama kuna kitu aliandika kwenye ‘peji’ yake yeye hakuona.Alisema
anachokumbuka ni kwamba aliongea naye (Esma) akiwa Hospitali ya Aga Khan
Aghakan, Dar.
“Huwa siongei na Esma mara kwa mara kwani sina sababu sana ya kuwa naye kwa kuwa si mume wala bwana’ngu.
“Pia sijawahi kukwaruzana naye, sasa kama kuna kitu alisema, mimi
namtafutia wanawake mumewe basi atakuwa anakosea kabisa,” alisema Wema.
No comments:
Post a Comment