Maelfu ya watu nchini Nepal wamelala
nje usiku kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba nchi hiyo jana
Jumamosi ambalo lilisababisha uharibifu mkubwa na kupotea kwa maisha.
Serikali ya Nepal inasema inaamini kuwa takriban watu 1500 wameaga dunia lakini idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka wakati makundi ya uokoaji yanapotafuta kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka.
Hali mbaya ya hewa inalikumba eneo hilo na watoa huduma za dharura wanasema kuwa huenda ikavuruga jitihada za uokoaji.
No comments:
Post a Comment