Wanamgambo wanaoaminika kuwa Al Shabaab wamemteka nyara chifu na gari la miraa katika eneo la Arabia, kaunti ya Mandera.
Viongozi wamesema washambuliaji walionekana kufahamu eneo hilo na pia Chifu waliyemteka nyara. Inasemekana kuwa Chifu huyo alikuwa akielekea Mandera wakati wa shambulizi hilo.
Awali katika idhaa yaa BBC Somali tuliweza kuzungumuza na mwakilishi wa kaunti katika wadi ya Arabia na kaweza kutuhakikishisa shambulizi hilo na vile vile alisema kuwa wanashuku wanamgambo wa Alshabab ndio waliofanya kitendo hicho.
Hadi sasa hakuna taarifa rasmi kutoka serikali kuhusiana na utekaji nyara na muda mfupi uliopita kulikuwa na taarifa isiyo thibitishwa kuwa chifu huyo ameuwawa na Alshabaab.
Kutokana na swala hili la Usalama wanasiasa jimbo la Mandera waliweza kuongea na wanahabari huku wakilaani kitendo hicho huku wakihimiza serikali kuimarisha usalama katika mkoa wa kaskazini mashariki mwa Kenya.
No comments:
Post a Comment