Wanafunzi katika chuo kikuu cha
Burundi mjini Bujumbura, wanasema kuwa serikali imewaagiza kufungasha
virago vyao na kuondoka chuoni hapo mara moja kwani chuo hicho
kinafungwa.
Watu watano wameripotiwa kufariki tangu kuzuka kwa ghasia hizo siku kadhaa zilizopita.
Umoja wa mataifa umeonya kuwa huenda taifa hilo likaingia katika lindi la mzozo wa kisiasa, iwapo ghasia hizo zitakithiri, mwezi mmoja tu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu hapo mwezi Juni.
Maafisa wakuu wa umoja wa mataifa na mwanadiplomasia wa Marekani, kwa sasa wanashauriana na serikali ya Burundi, ili kukabiliana na taharuki hiyo ya kisiasa.
Mapema polisi walitibua maandamano ya watu waliokuwa na lengo la kuweka vizuizi kwa raia Nkurunzinza kuwasilisha stakabadhi zake hii leo kama mgombea wa urais wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment