Mokoena aliyewahi kutamba na klabu za Blackburn
Rovers na Portsmouth zote za England ametua jijini juzi ambapo jana
alifanikiwa kuishuhudia Yanga ikitoa kipigo cha mabao 4-1 kwa Polisi
Moro.
Mokoena kwa sasa hana timu amesema yuko tayari kucheza Yanga kama klabu hiyo itakubaliana naye.
“Nimekuja kuwaangalia Yanga nimewaona leo (jana)
ni timu inayocheza soka safi, sijaja kufanya majaribio hapa kama Yanga
wananihitaji nipo tayari kufanya vipimo na kuwafanyia kazi nimeambiwa
wanashiriki mashindano ya Afrika,”alisema Mokoena.
Wakala Gibby Kelvic ndiye aliyemleta mshambuliaji
wa Yanga, Kpah Sherman, alisema ameamua kumleta Mokoena kufuatia uongozi
wa Yanga kumtaka kuwaletea beki mwenye uzoefu endapo watakubaliana
anaweza kusaini kuitumikia klabu hiyo msimu ujao.
“Niliambiwa wanahitaji beki,nimewaletea huyu
Mokoena ambaye haikuwa rahisi kukubali kuja hapa Tanzania, lakini
baadaye alikubali na leo (jana) ameiona timu na akaipenda,” alisema
Gibby.
No comments:
Post a Comment