Meneja
wa Sauti za Wananchi wa Twaweza, Elvis Mushi (kulia) akitoa ufafanuzi
katika mkutano huo. Kushoto ni Afisa Masoko wa Twaweza, Costantine
Magavilla.Viongozi mbalimbali wa taasisi na wanahabari wakifuatilia semina hiyo.
Taasisi ya Utafiti ya Twaweza imeandaa semina iliyowashirikisha watu
mbalimbali na taasisi binafsi kuhusiana na uhalifu na vurugu pamoja na
makundi ya vijana watakaosababisha vurugu kuelekea Uchaguzi Mkuu,
Oktoba, mwaka huu.Akizungumza kwenye semina hiyo iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar, meneja wa Sauti za Wananchi wa Twaweza, Elvis Mushi alisema kuwa wananchi wanakabiliwa na hofu kubwa ya makundi ya vijana wanaojitokeza kufanya mambo yasiyokuwa na msingi.
Alisema makundi hayo yamesababisha hofu kubwa miongoni mwa wananchi, hivyo aliitaka serikali na vyombo vinavyohusika kuhakikisha vinalinda usalama wa raia.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze alisema kuwa wananchi wengi wanajiona hawapo salama katika maeneo yao lakini bado wanakumbana na vitendo vya wizi kutoka kwa vijana wa mtaani.
Alitolea mfano wa vikundi vinavyotambulika kama vile Panya Road ambavyo kazi yake ni kuhatarisha usalama na vinaweza kuibua vurugu za kisiasa kwenye uchaguzi huo.
Hata hivyo, Eyakuze aliongeza kuwa katika kuelekea Uchaguzi Mkuu, jeshi la polisi linatakiwa kuwa makini katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.
Alisema kuwa hata wanasiasa watakaosababisha machafuko lazima wachukuliwe hatua kali kwani Twaweza inapinga vikali makundi yanayoweza kusababisha hali ya vurugu na ghasia miongoni wa wananchi.
No comments:
Post a Comment