Marekani, Umoja wa Matiafa, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika zina
mhimiza rais Pierre Nkurunziza wa Burundi kuheshimu katiba wakati
ghasia na maandamano yakiendelea nchini humo tangu uwamuzi wake wa
Jumamosi April 25 kutangaza anagombania tena mhula mwengine.
Rais Barack Obama amemtuma naibu waziri wa mambo ya nchi za nje kwa ajili ya demokrasia, haki za binadam na kazi Tom Malinowiski, hadi Bujumbura akiwa na ujumbe wa kuwahimiza wakuu wa nchi hiyo kutochukua hatua ambazo zitaweza kutumbukiza nchi hiyo katika hali isiyoweza kurekebishwa tena.
"Ujumbe wangu kwa wakuu wa Burundi ni kwamba muda haujapita bado kuonesha uwongozi, muda haujapita kuonesha ustahmilivu na kuepusha kutumia ghasia. Na muda haujapita kuwazuia baadhi ya vijana wenye silaha na wengine walohusika katika ghasia siku za nyuma. Msichukuwe hatua ambazo mtakuja kujuta."
Bw Malinowski anasema bado kuna muda na nafasi ya majadiliano, kwani anasema Burundi imeweza kufanya maendeleo makubwa katika kurudisha hali ya utulivu baada ya vita vibaya vya wenyewe kwa wenyewe karibu miaka 10 iliyopita.
Umoja wa Mataifa wapeleka ujumbe.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban ki Moon anatuma mwakilishi wake maalum kwa Kanda ya Maziwa Makuu huko Burundi Said Djinnit, kwa mashauriano na maafisa wa serikali, Rais Nkurunzinza na viongozi wa vyama vya siasa.
Katibu Mkuu Ban, amewataka wakuu wa idara za usalama wa Burundi kufanya kazi kwa weledi na kwa pande zote kuachana na ghasia na kuepuka hotuba zenye kuchochea chuki.
Mwenye kiti wa tume ya Afrika, Nkosazana Dlamini Zuma ametowa wito Jumapili kupitia ujumbe wa Twitter, kuwataka viongozi wa Burundi kujaribu kuonesha ustahmilivu kwa waandamanaji wanaopiga mhula wa tatu wa rais
Katibu mkuu wa zamani wa chama tawala cha CNDD-FDD, Hussein Rajabu
akiwa uhamishoni anasema ni jambo la kusikitisha yanayotokea lakini ana
uhakika warundi watapata ushindi katika kulinda mafanikio walopata tangu
makubaliano ya Arusha.
Watu wasiopungua sita wamefariki dunia wiki hii katika mapambano kati ya Polisi na waandamanaji katika mji mkuu Bujumbura, na maelfu ya warundi wameshakimbia hadi nchi jirani za Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakihofia ghasia zinaweza kuzuka tena nchini mwao.
Rais Barack Obama amemtuma naibu waziri wa mambo ya nchi za nje kwa ajili ya demokrasia, haki za binadam na kazi Tom Malinowiski, hadi Bujumbura akiwa na ujumbe wa kuwahimiza wakuu wa nchi hiyo kutochukua hatua ambazo zitaweza kutumbukiza nchi hiyo katika hali isiyoweza kurekebishwa tena.
"Ujumbe wangu kwa wakuu wa Burundi ni kwamba muda haujapita bado kuonesha uwongozi, muda haujapita kuonesha ustahmilivu na kuepusha kutumia ghasia. Na muda haujapita kuwazuia baadhi ya vijana wenye silaha na wengine walohusika katika ghasia siku za nyuma. Msichukuwe hatua ambazo mtakuja kujuta."
Bw Malinowski anasema bado kuna muda na nafasi ya majadiliano, kwani anasema Burundi imeweza kufanya maendeleo makubwa katika kurudisha hali ya utulivu baada ya vita vibaya vya wenyewe kwa wenyewe karibu miaka 10 iliyopita.
Umoja wa Mataifa wapeleka ujumbe.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban ki Moon anatuma mwakilishi wake maalum kwa Kanda ya Maziwa Makuu huko Burundi Said Djinnit, kwa mashauriano na maafisa wa serikali, Rais Nkurunzinza na viongozi wa vyama vya siasa.
Katibu Mkuu Ban, amewataka wakuu wa idara za usalama wa Burundi kufanya kazi kwa weledi na kwa pande zote kuachana na ghasia na kuepuka hotuba zenye kuchochea chuki.
Mwenye kiti wa tume ya Afrika, Nkosazana Dlamini Zuma ametowa wito Jumapili kupitia ujumbe wa Twitter, kuwataka viongozi wa Burundi kujaribu kuonesha ustahmilivu kwa waandamanaji wanaopiga mhula wa tatu wa rais
Hussein Rajabu azungumzia ghasia za Bujumbura
Watu wasiopungua sita wamefariki dunia wiki hii katika mapambano kati ya Polisi na waandamanaji katika mji mkuu Bujumbura, na maelfu ya warundi wameshakimbia hadi nchi jirani za Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakihofia ghasia zinaweza kuzuka tena nchini mwao.
No comments:
Post a Comment