Thursday, 30 April 2015

WATOTO WAFANYA MBAYA BABA NA MAMA ,,,>>


Mkono wa baba aliyeuliwa na mwanaye.

POLISI katika Jimbo la Enugu, Nigeria, wanachunguza vifo ambapo wanaume wawili wasiokuwa ndugu, waliwaua baba na mama zao katika matukio mawili tofauti.

Mauaji hayo yalitokea Aprili 26 Jumapili iliyopita na Aprili 27 Jumatatu ya wiki hii sehemu tofauti ambapo muuaji wa kwanza, Chijioke Onyeke, alimkata baba yake kwa panga mnamo saa 12 jioni katika ugomvi usiofahamika chanzo chake katika kijiji cha Umuogboagu kaskazini mwa nchi hiyo.

Mtu huyo alifia katika hospitali ya St. Mary, kutokana na majereha ambapo mtuhumiwa alikamatwa.
Katika tukio jingine, Chidi Agbo, kutoka kijiji cha Igboeze, kaskasini mwa nchi hiyo, alimpiga mama yake hadi kumwua ambapo pia sababu ya kufanya hivyo haijulikani.
Chidi naye yuko mikononi mwa polisi.

source ..  MTANDAO WA PULSE

No comments:

Post a Comment