Ukrain inasema kuwa mmoja wa
wanajeshi wake ameuawa na wengine 14 kujeruhiwa kwenye mashambulizi
mapya yanayoendeshwa na waasi wanaoiunga mkono Urusi mashariki mwa nchi.
Serikali inawalaumu waasi kwa kutumia makombora na silaha zingine nzito zilizopigwa marufuku wakati wa makubaliano ya kusitisha vita.
Makubaliano hayo yalistahili kuwa nchini ya uangalizi wa idara ya usalama ya muungano wa ulaya lakini waasi wameizuia idara hiyo kuzuru eneo ambalo inasema kuwa ina silaha nzito.
No comments:
Post a Comment