RAIS KENYATA
Rais Uhuru Kenyatta, amewasimamisha
kazi wakuu wawili wa shirika linalopambana na ufisadi nchini humo, siku
moja tu baada ya bunge kupitisha mswaada inaowalaumu kwa uzembe na
utepetevu.
Waku hao ambao ni mwenyekiti, Mumo Matemu na naibu wake Bi Irene Keino wamesimamishwa huku uchungunzi ukianzishwa dhidi yao kuhusiana na tuhuma za kuzembea kazini na kutumia vibaya mamlaka yao.
Tangazo hilo limefanyika chini ya mwezi mmoja baada ya ripoti kutoka kwa tume hiyo kuwasilishwa kwa Rais Kenyatta iliyosababishwa kusimamishwa kazi kwa mawaziri wanne wa serikali ya Uhuru Kenyatta na maafisa wengine 12 wakuu serikalini, huku uchunguzi dhidi yao ukianzishwa.
Wanatuhumiwa kuhusika na ufisadi.
No comments:
Post a Comment