Monday, 27 April 2015

BAYERN MUNICH MABINGWA UJERUMANI ...

  

Klabu ya soka ya Ujerumani Bayern Munich ya Ujerumani imenyakuwa taji la ligi kuu ya nchi hiyo kwa mara ya tatu mfululizo huku shukrani zikienda kwa klabu ya soka ya Borussia Monchengladbach kwa kuichabanga Wolfsburg kwa bao 1-0 siku ya jumapili.

Kipigo hicho walichokipata Wolfsburg ndicho kilichofanya mashabiki wa Bayern kusherehekea ubingwa kwa kuwa timu hiyo ndio inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wakiwa na pointi 61, wakati vijana wa Pep Guardiola yaani Bayern Munich wawakiwa kileleni kwa pointi 76 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kutokana na idadi ya mechi zilizobaki.

Lakini wachezaji wa wa Bayern hawatokuwa na muda wa kutosha kusherehekea ubingwa huo kutokana na majukumu mazito yanayowakabili ya klabu bingwa Ulaya ambapo watavaana Barcelona mnamo May 6 katika mchezo wa nusu fainali.

No comments:

Post a Comment