MWANDISHI WETU
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Tamrina Poshi
‘Amanda’ amefunguka kuwa baada ya kukanusha kuwa hana ugonjwa wa Ukimwi,
mpenzi wake amemcharukia kweli akihoji kwa nini akanushe kama hana?
Akizungumzia tukio hilo, Amanda alisema baada ya gazeti la Ijumaa la
wiki iliyopita kuripoti akimchana shabiki aitwaye Joel ambaye aliandika
mtandaoni kuwa mwigizaji huyo anatumia vidonge vya ARV ili kuongeza
nguvu za kuishi, ndipo mchumba wake akacharuka.
“Baby alicharuka kweli akadhani labda pengine ni kweli wakati mimi
nimepima na majibu yangu ni mazuri, nilimuelewesha kwamba nilimchamba
yule shabiki ambaye aliropoka tu bila ushahidi, nashukuru alinielewa na
sasa tuko poa,” alisema Amanda.
No comments:
Post a Comment