Shirikisho la soka barani Afrika, CAF imeondoa vipengee vinavyodhibiti umri wa wagombea viti vya kamati kuu.
Viongozi wote wa mashirikisho ya kandanda 54 ya bara la Afrika walikubali mapendekezo hayo ambayo yaliondoa kipengee hicho.
Kipengee hicho kilikuwa kinamzuia mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka 70 kushikilia wadhfa wowote katika shirikisho.
Viongozi hao walitumia kisingizio cha uwiano wa kanuni zao na zile za shirikisho la soka duniani FIFA.
Hayatou, 68, sasa atakuwa huru kuwania awamu nyengine mwishoni mwa mwaka wa 2017.
Hayatou anatarajia kuwania kiti hicho cha urais ambayo itamruhusu kuongoza hadi atakapotimu miaka 75 mwaka wa 2021.
Awali wapinzani wa wa kiongozi huyo wa CAF walidai kuwa alikuwa akibadilisha sheria kwa madhumuni ya kumnyima mpinzani wake uwezo wa kushindana naye.
Aidha CAF ilipopitisha sheria ya kumtaka muaniaji kiti cha urais kuwa mwenyekiti wa kamati kuu washindani wengi waliona kama ni njama ya kuzuia upinzani wa utawala wake.
Sheria hiyo haipo katika shirikisho kuu la FIFA.
Raiya huyo wa Cameroon ameliongoza shirikisho la Soka Afrika tangu mwaka wa 1988.
Aidha anahudumu pia kama naibu rais wa FIFA ambaye ni mmoja kati ya viongozi waliohudumu kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment