JAMAL MALINZI
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Jamal Malinzi amewatakia kila la kheri wawakilishi pekee wa
Tanzania kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika Young Africans, katika
mchezo wa marudiano dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe utakochezwa siku
ya jumamosi kwenye uwanja Mandava uliopo Gweru Bulawayo.
Endapo Young Africans itafanikiwa kuwatoa FC Platinum itaingia katika hatua ya 16 bora na itakutana na mshindi kati ya timu za Benifica de Luanda ya Angola au Etoile du Saleh ya Tunisia.
No comments:
Post a Comment