Kulikuwa na kaburi la muda,misalaba na mishumaa vilivyowekwa katika viwanja vya mji mkuu wa Kenya ,Nairobi ili kuwakumbuka wanafunzi waliouawa katika shambulio la chuo kikuu cha Garissa ,shambulio ambalo lililotekelezwa na mwanamgambo aliyekuwa na silaha kutoka katika kundi la Al Shabaab,mwishoni mwa wiki iliyopita.
Picha za waathirika wa shambulio hilo wapatao mia moja na arobaini na nane ziliwekwa bayana katika ibada ya mkesha, katika maadhimisho ya kuhitimisha maombolezo ya kitaifa nchini humo yaliyodumu kwa muda wa siku tatu.
Garissa kwenyewe watu wapatao elfu mbili walikusanyika katika mkutano wa hadhara ,nayo mahakama kuu mjini Nairobi imetoa mwezi mmoja zaidi kwa polisi kuwahoji washukiwa sita wa tukio la Garissa ambao wanashukiwa kuwapelekea silaha wauaji waliotekeleza tukio lile.
No comments:
Post a Comment