Tuesday, 7 April 2015

MIAKA 10 YA MAFANIKIO YA JAKAYA ... >>

 

SERIKALI ya awamu ya nne inajivunia mafanikio iliyoyapata tangu kuingia madarakani mwaka 2005 na kuweka msingi imara wa nchi katika kutekeleza Mkakati wa Maendeleo wa Mwaka 2025 ambao unalenga kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Aidha, Rais Jakaya Kikwete anayeiongoza awamu hiyo, amesema anatumaini uchaguzi mkuu ujao utakaotoa wabunge, madiwani na rais ya awamu ya tano unaotarajiwa kufanyika Oktoba , utakuwa huru na wa amani.
Natumaini tutafanya uchaguzi huru, haki na amani ili niweze kumkabidhi urais mrithi wangu katika hali ya utulivu,” Rais alisema.
Rais aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Washington DC wakati akitoa mhadhara katika kituo cha Kimataifa cha Woodrow Wilson.
Naamini mrithi wangu atayaendeleza na kujifunza kutokana na mafanikio haya na kuendeleza kutoka pale tutakapoachia,” Rais Kikwete alisema na kuongeza anatarajia kuwa Tanzania itakuwa na sera na sheria ya kusimamia Gesi na mapato yake kwa vile inatarajiwa kuanza kupatikana ifikapo mwaka 2020.

No comments:

Post a Comment