Tuesday, 7 April 2015

ADHABU YA KIFO KWA WA AUSTRALIA WAWILI NA MFARANSA ATLAOUI NCHINI INDONESIA ...>>

   Akiwa madarakani tangu mwezi Oktoba mwaka jana, rais Joko Widodo, aliahidi kupambana dhidi ya biashara ya madawa ya kulevya.

Rufaa ya raia wawili wa Australia waliohukumiwa adhabu ya kifo Indonesia kwa kupatikana na hatia ya kufanya biashara ya mihadharati imefutiliwa mbali Jumatatu wiki hii.

Rufaa ya raia wawili wa Australia waliohukumiwa adhabu ya kifo Indonesia kwa kupatikana na hatia ya kufanya biashara ya mihadharati imefutiliwa mbali Jumatatu wiki hii.

Mahakama inayoshughulikia masuala ya Utawalaimebaini kwamba haina uwezo wa kutathmini rufaa yao kwa msamaha. Raia hao ambao walihukumiwa mwaka 2006, walikua wanatazamiwa kunyongwa hivi karibuni, huku raia wengine wanane wa kigeni wakisubiri maamuzi ya mahakama. 

Hatima ya raia wa Ufaransa Serge Atlaoui, ambaye ni miongoni mwa wanane hao waliohukumiwa adhabu kifo, bado haijajulikana.

Waziri wa kigeni wa Australia, Julie Bishop, amesema ataendelea kutetea wafanyabiashara hao wawili wa zamani wa heroin ambao walihukumiwa adhabu ya kifo mwaka 2006, na mamlaka ya Indonesia. Hoja yake kuu imesalia ile ile: Myuran Sukumaran, mwenye umri wa miaka 33, na Andrew Chan, mwenye umri wa miaka 31, ni wafungwa mfano na wamekua wakijuta.

Miezi ya hivi karibuni, serikali ya Australia imekua ikijaribu kuishawishi serikali. Tonny Abbott amekua akiomba raia wake hao wawili wapewe msamaha kulingana na msaada Australia iliyoitolea Indonesia baada ya nchi hiyo kukumbwa na dhoruba ya Tsunami mwaka 2004.

Kwa wakati huu, mawakili wa raia mahabusu hao wanajaribu kuokoa muda. Mawakili hao wanatazamia kukataa rufaa dhidi ya uamzi wa kukataa kupewa msamaha wateja wao.

No comments:

Post a Comment