Mwakilishi wa Jimbo la Bububu Zanzibar Mhe Hussein Ibrahim Makungu
akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tuhuma zanazoenezwa
kwamba gari lake aina ya fuso kuhusika na kuwashambulia Wanachama wa CUF
wakati wakirudi Mkutanoni makunduchi, Akitowa maelezo kwa waandishi wa
habari katika ukumbi wa salama bwawani amesema gari hiyo iliotumika
katika tukio hilo haiko katika milki yake, hiyo gari iliohusisha na
tukio hilo aliiuzwa karibu sasa miaka minane na kumulikiwa na mtu
mwengine akiwa bado hajalifuta jina la Bhaa Staily,
Amesema analaani kitendo hicho waliofanyiwa wananchi hao.
Mhe. Hussein Ibrahim Makungu, akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo na
kusema gari lajimbo siku hiyo halikutoka kwenda popote na kuegeshwa
katika hospitali ya Kibweni KMKM, anashangaa kusikia kauli hiyo ya
kulihusisha gari hilo na tukio na kueleza kwa waandishi wa wahabari
Zanzibar
No comments:
Post a Comment