Mashabiki wa timu ya SIMBA
Ligi kuu Tanzania Bara itaendelea
wikiendi hii huku kocha wa mabingwa wa zamani wa Tanzania Bara, Simba,
Mserbia Goran Kopunovic akiipigia mahesabu ya ushindi timu ya Kagera
Sugar katika uwanja wa Kaitaba hapo Jumamosi.
Simba ina pointi 32, ikiwa ya tatu katika msimamo, ambapo wapinzani wao wa jadi, Yanga wanaongoza ligi wakiwa na pointi 40 huku Azam wakiwa nafasi ya pili na pointi 36.
Mechi nyingine za Jumamosi ni Coastal Union itakapocheza na Tanzania Prisons mkoa wa Tanga, Kaskazini mwa Tanzania.
Akizungumza leo mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo yanayo endelea kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly mjini Tanga,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kikubwa zaidi wanachojivunia ni kuendelea kuimarika kikosi hicho.
Amesema kuwa mipango yake mikubwa ni kuiwezesha timu hiyo kupata matokeo mazuri katika mechi zote zilizosalia ikiwemo kuwataka wachezaji kutimiza wajibu wao wa kuipa ushindi timu hiyo.
Amesema kuwa dhamira yao kubwa ni kupambana kufa na kupona ili kumaliza ligi hiyo wakiwa nafasi tatu za juu kwenye michuano hiyo ambayo msimu huu imeonekana kuwa na upinzani mkubwa.
Mechi nyingine ni Ndanda FC vs Mbeya City (Mtwara),JKT Ruvu vs Ruvu Shooting ( Mabatini-mkoa wa Pwani),
No comments:
Post a Comment