MAREHEMU M. MHITA
MBONI MTOTO WA MAREHEMU
ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Hali ya Hewa (TMA),Dk. Mohamed Mhita, amefariki dunia.
Dk. Mhita
ambaye pia ni mume wa Mbunge wa Kondoa Kaskazini, Zabein
Mhita, anatarajiwa kuzikwa leo baada ya
kuwasili kwa mkewe, aliyeko India kwa matibabu.
Akizungumza na waandishi wa habari,
mtoto wa marehemu, Muhaji
Mhita alisema baba yake aliugua maralia, Jumatatu alfajiri na kupelekwa
hospitali, ambapo alifariki usiku.
Alisema walipofika
hospitali walibaini kuwa shinikizo la damu lilikuwa juu na alikutwsa na mauti saa nne usiku.
Muhaji alisema Jumapili usiku, baba yake alimjulisha
juu ya hali yake, ndipo ilipofika alfajiri aliamua kumpeleka
hospitali.
“Baba atazikwa kesho (leo), ila bado hatujapanga kama tutamzika Handeni au hapa Dar es Salaam, kwani tunamsubiri mama ambaye yuko nje ya nchi na leo (jana), usiku atakuwa ameshafika,” alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mboni Mhita, ambaye ni
mtoto wa marehemu alisema amesikitishwa na kifo cha baba yake na kimewaachia simanzi
kubwa.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi, akizungumza
na Uhuru kuhusiana na kifo hicho, alisema ni pigo kwa taifa kwa sababu bado
lilikuwa linahitaji mchango wake.
Alisema licha ya Dk. Mhita kustaafu utumishi wa umma,
walikuwa wakishirikiana naye katika mambo mbalimbali, ikiwemo ushauri na
maelekezo kwa watumishi wa mamlaka.
“Tulishirikiana naye sana, kutokana na uzoefu wake muda wote wa utumishi wake wa mafanikio hapa TMA, hivyo tulikuwa tunatafuta mafanikio hayo pia kupitia yeye,” alisema.
Dk. Agnes ambaye alipokea kijiti kutoka kwa Dk. Mhita
kuiongoza TMA, alitoa pole kwa familia na Watanzania kwa ujumla kutokana na
msiba huo.
No comments:
Post a Comment