Dar es Salaam. Siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kusema kuwa nafasi hiyo ni kadhia na kazi ngumu, baadhi ya wanasiasa waliotangaza nia ya kuwania nafasi hiyo wamesema wanafahamu changamoto hizo na kwamba kauli hiyo inazidi kuwapa nguvu na hamasa ya kuendelea na mchakato huo.
Wiki iliyopita, Rais Kikwete akiwa Marekani,
wakati akihutubia kwenye taasisi ya Wood Wilson
International Center for Scholars alielezea mafanikio na changamoto alizokumbana nazo wakati wa uongozi wake wa miaka 10 unaomalizika Oktoba, mwaka huu na kusema:
International Center for Scholars alielezea mafanikio na changamoto alizokumbana nazo wakati wa uongozi wake wa miaka 10 unaomalizika Oktoba, mwaka huu na kusema:
“Wakati unaingia Ikulu unakuwa na shauku kubwa
sana pamoja na furaha ya ushindi, lakini hakika urais ni kadhia kubwa.
Ukipata fursa ya kuwa rais kwa awamu mbili kama mimi nadhani zinatosha
kabisa.
Nimefanya mengi kwa nchi yangu atakayekuja ataendeleza nilipoishia.”
Nimefanya mengi kwa nchi yangu atakayekuja ataendeleza nilipoishia.”
Kauli hiyo ya Rais Kikwete imekuja wakati makada wa CCM wakipigana vikumbo kuwania urais.
Miongoni mwa wanasiasa waliotangaza na waliotajwa
katika kinyang’anyiro hicho cha kurithi kiti kitakachoachwa wazi na Rais
Kikwete ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Mbunge wa
Nzega, Dk Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na
Uratibu), Stephen Wasira, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, January Makamba na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Pia wamo, Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel
Nchimbi, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na aliyekuwa Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Msimamo wa January
Akizungumza jana kuhusiana na kauli hiyo ya January alisema kauli hiyo inampa hamasa kwa nia yake ya kutaka kuwania urais.
“Nilitangaza nia hiyo huku nikiwa nafahamu kwa
asilimia 100 uzito wa jambo hilo... kufahamu changamoto hizo ndiyo moja
ya vitu vilivyonisukuma kuchukua uamuzi huo,” alisema.
Alisema moja ya changamoto ambazo ameshakumbana nazo alisema: “Kwanza mimi nina bahati sana. Wakati nikiwa msaidizi wa Rais kipindi anagombea nafasi hiyo, nilipata fursa ya kutembea naye nchi nzima na kuona mambo mengi.”
Mbunge huyo wa Bumbuli, alisema haikuwa kazi rahisi kufanya kampeni za kuhamasisha Watanzania wampigie kura Rais Kikwete... “wakati ule tulikuwa tunatembea katika maeneo mbalimbali nchini. Ukiwa umesimama jukwaani unaona sura za watu zilivyojawa na shauku… pale nilijifunza na kuona ukubwa wa changamoto za uongozi.
Nimebahatika pia kuona changamoto mbalimbali ambazo uongozi wa sasa umekumbana nazo kwa kipindi nilichowatumikia hadi sasa. Hiyo ni nafasi nzuri ya mimi kujifunza na kufahamu ni namna gani ninaweza kukabiliana nazo.
No comments:
Post a Comment