Monday, 6 April 2015

MEMBE AMSHUGHULIKIA PINDA ....>>Fatma Murshid‎ TANURU LA FIKRA saa 16 zilizopita ameandika ..

             Tokeo la picha la MEMBE   Tokeo la picha la PINDA

* Atumia Milioni 20 kummaliza Sasa sio siri tena kuwa Waziri wa Mambo ya nchi za nje na mahusiano ya Kimataifa Mhe. Bernad Membe na Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda wapo kwenye ugomvi mkubwa unaoweza kutoana roho wakati wowote ule. 

Pinda na Membe wote wapo kwenye harakati za kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambao ugomvi wao umekolezwa zaidi na tamasha kubwa la kiinjili maarufu kama tamasha la pasaka. 

Mnyetishaji wetu (jina linahifadhiwa) anadai ya kuwa tamasha la mwaka huu la kusherehekea kutimiza miaka 15 alialikwa Pinda aje kuwa mgeni rasmi ili aje kutimiza ahadi yake aliyoitoa mwaka jana ya kuchangia milioni 20 kwa kwaya mbalimbali na badala yake ghafla uamuzi ukabadilishwa na kutolewa Pinda na kuchomekwa Membe.

Inasadikiwa mara baada ya siri kuvuja juu ya deni la ahadi ya Pinda alijitokeza mtoto wa Rais Kikwete aitwaye Ridhiwani Kikwete na kukutana na uongozi wa Msama promotion ambao ndio waandaji wa tamasha hilo la kuwaambia yupo tayari kulilipa deni hilo la Pinda kwa masharti ya Membe kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo.

Ridhiwani ambaye anamwita Membe baba mdogo kutokana na kuwa mtoto wa nje wa Babu yake ambaye ndiye aliyemzaa Baba yake Jakaya Kikwete aitwaye Mzee Mrisho Kikwete ameapa kuendelea kupambana na Pinda ili kumtengenezea mazingira ya kuingia ikulu baba yake mdogo, Membe. 

Membe naye akatia nguvu zaidi kwa kutoa kiasi cha Tsh milioni 10 kama shukrani yake kwa Msama ya kuchaguliwa kuwa mgeni rasmi. Kitendo hicho cha kuenguliwa kilimuudhi sana Pinda ambaye amehaidi kumlipizia kisasi kwenye Bunge la bajeti kwa kuikwamisha bajeti ya wizara inayoongozwa na Membe.
Mytake: Tuacheni movie ya kuingia magogoni iendelee, sie yetu macho

No comments:

Post a Comment