Serikali ya Kenya imemtambua mmoja
ya wapiganaji waliohusika katika mauaji ya chuo kikuu cha Garissa kwamba
ni mtoto wa afisa wa serikali.
Mtu huyo sasa ametambulika kama mwana wa kiume wa Chifu wa eneo la Kazkazini mashariki mwa kenya.
Alidaiwa kutoweka na ilihofiwa kwamba amesafiri nchini Somalia.
Wizara ya ndani inasema kuwa wapiganaji wote waliuawa siku ya alhamisi.
Washukiwa wengine watano wamakamatwa kufikia sasa kwa kuhusishwa na mauaji hayo ambayo ni mabaya zaidi kuwahi kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa Alshabaab.
No comments:
Post a Comment