Wednesday, 8 April 2015

RAIA MWEUSI MAREKANI AUWAWA NA AFISA WA POLISI MZUNGU ..>>>

Picha hii imepigwa kupitia videoiliyorushwa hewani tarehe 7 Aprili mwaka 2015 ambayo inamuonyesha Michael Slager, polisi katika jimbo la North Carolina, akiugeuza mwili wa Walter Scott, baada ya kumfunga pingu.
Afisa wa polisi wa jimbo la Caroline ya Kusini, nchini Marekani ameshatkiwa kwa mauaji. Afisa huyo wa polisi mzungu amemuua dereva mweusi, raia wa Marekani kwa kumpiga risasi nane mgongoni.

Tukio hili linatokea wiki kadhaa baada ya machafuko ya kikabila katika mji wa Ferguson pamoja na wimbi la hasira lililoikumba Marekani kufuatia kifo cha Mike Brown, raia mweusi wa Marekani aliyeuawa na afisa wa polisi mzungu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Washington, Anne-Marie Capomaccio, tukio hili lilitokea Jumamosi Aprili 4 mwaka 2015, katika mji wa North Charleston, katika jimbo la Caroline ya Kaskazini. Mkasa huo uliwekwa wazi katika video iliyorushwa na wenzetu wa New York Times Jumanne Aprili 7, baada ya kurekodiwa na shahidi mmoja. Video hiyo inamuonesha Walter Scott, mtu mwenye umri wa miaka 50, akikimbia akiwa mbele ya afisa wa polisi mzungu, ambaye alikua akivalia sare ya polisi ya Marekani, huku akiwa ameshikilia bunduki mkononi.

Mbio za wawili hao zilisitishwa mara moja tu, baada ya afisa huyo wa polisi kumpiga Walter Scott risase nane mgongoni. Baada ya Walter Scott kudondoka, afisa huyo wa polisi alimsogelea Scott na kumtupia pingu mgongoni.

Afisa huyo wa polisi Thomas Slager amejitetea akisema kwamba Mmarekani huyo mweusi, alikua akiendesha gari, na baadae alisimamishwa na polisi kwa minajili ya ukaguzi, lakini alipinga amri hiyo, na kumuibia polisi kifaa chake cha kazi. Slagger Thomas amesema alimpiga walter Scott risasi kwa sababu alijihisi kuwa usalama wake uko hatarini. Lakini utetezi wake huo hauonekani kwenye video.

Hata hivyo Thomas Slager ameshtakiwa kwa mauaji. Anakabiliwa na adhabu ya kifo au kifungo cha miaka 30 jela. Hali ya taharuki imetanda katika jimbo la California ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment