Thursday, 2 April 2015

TIMU YA NGUMI TANZANIA 2015 HII HAPA ..>>

                 

Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) limechagua wachezaji wa timu ya Taifa ya Ngumi 2015 ikishirikisha wachezaji wengi walioshiriki Katika mashindano ya kimataifa yaliyoshirikisha timu za taifa kutoka Uganda na Kenya, mashindano yaliyomalizika Dar es Salaam hivi karibuni.

Katibu mkuu wa BFT Makore Mashaga amesema mabondia waliochaguliwa kwa sasa taratibu za kuombewa ruhusa katika timu zao zinafanyika na taratibu hizo zitakapo kamilika watatakiwa kuanza mazoezi kabla ya tarehe 15.04.2015, kwa ajili ya kushiliki mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa hasa mashindano ya Michezo ya Afrika (All African Games) yatakayofanyika kuanzia Septemba 4-19, Congo Brazzaville
Pia watashiriki mashindani ya bingwa wa Dunia (AIBA World Boxing Championships) yatakayofanyika kuanzia Octoba 5-18 Doha Qatar.
Mabondia waliochaguliwa kwa uzito wao ni kama ifuatavyo:-
49 kgs L/FLY
• Mohamed Mzeru –JKT
• Maulid Athumani-
• Ibrahim Abdalah – Magereza.
52 Kgs Fly Weight.
• Juma Ramadhani- Temeke
• Said Hofu- JKT
56 Kgs Bantam Weight
• Ahamad Furahisha- JKT
• Bon Mlingwa- JKT
60 Kgs Light weight.
• Elias Mkomwa- JKT
• Bosco Bakari- JKT
• Fabian Gaudence- NGOME

No comments:

Post a Comment