Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania (TMA) imewataka wananchi kutojisahau kwani mvua ngingine kubwa zinatarajia kunyesha hivi karibuni. Hivi karibuni mvua kubwa zimenyesha maeneo mbalimbali ukanda wa pwani ikiwemo jiji la Dar es salaam na kusababisha mamia ya wananchi nyumba zao kuingia maji na kuharibu baadhi ya katika nyumba hizo.
Akizungumza katika baraza la wafanyakazi wa mamlaka ya hali ya hewa mkoani Morogoro Mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa nchini Dr. Agnes Kija...zi alisema kutokana na mabadiliko ya mfumo wa hali ya hewa ni muhimu wananchi kufuatilia taarifa za utabiri wa hali ya hewa ili wachukue tahadhari hasa kipindi hiki chenye mvua nyingi za masika.
Kwa upande wa mkuu wa wilaya ya mvomero Bw. Festo Kiswaga amelitaka mamlaka ya hali ya hewa kutoa taarifa za utabiri katika lugha nyepesi ili kuwezesha wananchi kulewa na kuwasaidia wakulima kupata taarifa za hali ya hewa kwa haraka ili watumie vizuri misimu ya kilimo.
No comments:
Post a Comment