Saturday, 4 April 2015

WANA CCM WAKIMNADI LOWASSA FULL FORCE ...


UKWELI KUHUSU SAKATA LA RICHMOND
Hii ni hoja ambayo kila uchao yeyote ambae atakua anampinga Edward Lowassa basi ndio funguo ya kuanzia popote atakapo simama ,hii kashfa kwa Lowassa ilianza muembe Yanga na Dr. Slaa aliopo toa orodha ya kwanza ya mafisadi hadi katika magazeti na watu kukaa hadi vikao wakitaka jina la Lowassa na bahati mbaya jina la Lowassa halikuwemo wakilenga atajwe katika scandal ya DAWASCO na kizuri zaidi serikali ilishinda katika kesi ile kwa maamuzi magumu ya Lowassa mpaka akahoji katika kikao cha ndani NEC mbele ya mwenyekiti kipi nilikifanya usicho kijua? Na huu ndio muendelezo wa mashambulizi hadi katika scandal iliyoitwa Richmond. Baada ya kujiuzulu kwa kiongozi huyu 2008 nilifuatilia sinema ile kwa umakini na nilishangazwa kuona kesi iliyofunguliwa dhidi ya Richmond na kuelezwa kuwa kampuni hii haipo na wala haijawahi kuwepo inashindaje kesi na mashauri yake yote yaliyo funguliwa dhidi yake ?, pili inakuwaje serikali inakubali mitambo inauzwa kwa DOWANS na baadae SYMBION kwa baraka za baraza la mawaziri?, inakuwaje mitambo hiyo inagharimu pesa za wamarekani ambao tunaamini wapo makini kwa waziri wao wa mambo ya nje H. Clinton na Rais wa Dunia Barack Obama wanaikagua kwa ziara ya gharama za fedha za Wamarekani?. Jibu hapa vita dhidi yake na mipango ilikwama na wanaposema fisadi alifisadi nini ? au ndio trolling mitandaoni dhidi yake?


Tokeo la picha la LOWASSA


No comments:

Post a Comment