YANGA TEAM
Sasa ni wazi kuwa wawakilishi wa
Tanzania katika michuano ya vilabu ya kombe la Shirikisho barani Afrika,
Yanga watacheza na Etoile du Sahel ya Tunisia katika raundi ya pili ya
michuano hiyo.
Vigogo hao wa Tunisia, wenye uzoefu wa kucheza michuano mikubwa Afrika, imepata nafasi ya kucheza na Yanga baada ya kutoka sare ya 1-1 na timu ya Benfica de Luanda. Katika mechi ya kwanza, Watunisia walishinda 1-0.
Kocha wa Yanga, Mdachi Hans Pluijm atakuwa na kibarua cha ziada kuwahkikisha wanasonga mbele huku nahodha wake, Nadir Haroub “Cannavaro” akisema wapo tayari kucheza na timu yoyote katika michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment