Bi JOYCE MUJURU
Aliyekuwa makamu wa rais nchini Zimbabwe Joice Mujuru amefukuzwa katika chama tawala ZANU-PF.
Bi Mujuru alipigana vita vya Guerilla pamoja na Mugabe miaka ya sabini dhidi ya uongozi wa weupe na alionekana kama mrithi wake,kabla ya kukosana naye mwaka uliopita swala lililomfanya kufutwa kazi kama makamu wa rais mnamo mwezi Disemba.
Waandishi wanasema alishtumiwa sana na mke wa Mugabe, Grace ambaye anaongoza wanawake katika chama hicho.
No comments:
Post a Comment