Saturday, 4 April 2015

SEREKALI YAFUNGA CHUO GARISA BAADA YA MAJANGA YA KUUWAWA WANAFUNZI NA AL SHAABAB ...

  
                                  CHUO CHA ''MAJANGA'' GARISA NCHINI KENYA

Wanafunzi katika chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya wanatarajiwa kupelekwa chuoni humo ili kundoa vitu vyao kabla ya kupelekwa nyumbani.

Serikali ya Kenya imefunga chuo hicho kufuatia shambulio la siku ya alhamisi ambapo watu 150 waliuawa.
Uchunguzi kuhusu tukio hilo unandelea na watu wawili zaidi wamekamatwa.

Walioshuhudia wanasema kuwa wale waliovamia chuo hicho walizungumza lugha ya kiswahili lakini walionekana kupata ushauri kwa njia ya simu za mkononi.

Rais wa Marekani Barack Obama amekitaja kitendo hicho kuwa cha kinyama na kuahidi msaada wake kwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

No comments:

Post a Comment