Saturday, 28 February 2015

R.I.P Capt ........


BORIS NEMTSOV APIGWA RISASI NA KUFA URUSI .....

 

 Boris Nemtsov mwanasiasa maarufu na kiongozi wa upinzani ameuwawa kwa kupigwa risasasi mjini Moscow .

Boris alipigwa risasi nne na watu wasiojulikana akiwa ana tembea mbele ya malengo ya serikali ,  watu hao walikua kwenye gari ndogo na walimlenga kwa nyuma .

Boris amewahi kua naibu waziri mkuu katika utawala wa Rais Boris Yeltsin na amekuwa akimpinga vikali Rais Vladimir Putin .

WATU 14 WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE 2000 WA MAPOTEZA MAKAZI KUTOKANA NA MAAFURIKO HUKO MADAGASCAR


Antananarivo

Friday, 27 February 2015

NDEGE YA KIVITA YA TANZANIA YAANGUKA MWANZA ....

  

Taarifa zaidi wadau zipo kwa wenzetu muchuzi , udaku, JF ... 


Kikosi cha kwanza cha askari wa kichina kikiingia Sudan kusini ...

MTANGAZAJI MAARUFU WA RADIO 5 APORWA MKE KWA NGUVU NA WAPAMBE WA DIAMOND ....





Beautiful wozn' they ....  !




Mtangazaji maarufu zaidi wa kanda ya kaskazini JULIUS KAMAFA aka Mafa Mafa ... ameporwa mke na wapambe wa msanii maarufu Dimond. ..

Katika picha ya harusi mpambe wa Diamond Rommy Jones anaonekana kufurahia sana wakiwa katika picha ya pamoja na mke wa mshkaji wetu na ambae juzi juzi alituzalia ka lito Brian ....

Mafa Mafa amedai hakukuwahi kutokea mikwaruzano na mkewe hata kwa bahatimbaya na kwamba mpaka sasa haamini kilichotokea .

Mama Brian aliniaga kua anakwenda kumsalimia mama yake dar ila sikujua kua kulikua na mpango kama huu unaendelea , cjui nini kimetokea bro. ..dah alisema kwa huzuni Mafa Mafa ... oyaa Diamond eeh! Mbona unazengua man ? Tabia gani hizi mnafanya ?? Unabifu gani na Kamafa ?? Huyo Dimond 2 hapo na mjombaako anafanya nini ? Mliwah kua na bifu na Kamafa ??

Sio poa ka Diamond ulijua kua Mwinyi anaenda kumuoa Liz wakati wote mnajua Liz anaishi na Mafa na wana mtoto .... sio poa ..

Oi badae. ..

NIACHE NIMALIZIE YA WA GONGA KOKOTO KINA MAMA JIJINI DAR .... INAUMA SANA !

 
Leo nitamalizia kasehemu ka mazungumzo yangu na kina mama wa Mbezi mbuyuni pale .. 
Huyu ni bi Fatma aliezea kisa kilichonisikitisha sana .. 
Huyu dem bana ana watoto wawili mume alimkimbia siku nyingi sasa .. mwanangu dem kapitia maisha yote .. anakwambia amewahi kuuza kwichi kwichi .. akakutana na nunda linakitu kama mguu wa mtoto ( her exactly words ) anakwambia kote kote ingemchana na jamaa anataka kula tope .. dem kashapewa laki na hamsini mapemaa na kamwachia best yake .. huku nako kitu kakuta over size , jamaa anadai chake au mzigo .. pesa ipo kwa shogaake na dem alafu home kunadaiwa kero imezidi kaamua kutoka akatafute cha watu  ...  Weee ! Usombe kujua kilichotokea na ndio sababu ya kuja kupasua mawe a wee kuishi ... doh.
Kumbuka huyu msichana ana watoto wawili aliyoachiwa na mume alimkimbia kwa ugumu wa maisha .
     
 
Huyu ni mimi na hii ndio ndoo ambayo ukigonga kokoto zikajaa hapa unalipwa shilingi Mia mbili za tanzania , katika kipindi hiki cha joto kali hapa dar ... jiulize watu hawa wanaishije ... Inauma sanaa !

Oi ... badae ...

KUBANDIKIZA KICHWA SASA KUNAWEZEKANA .. DYUUU...!

 
Unaposikia habari hii utadhani ni maudhui ya filamu ya kutisha ,lakini wanasayansi wanaamini upasuaji wa upandikishaji wa kichwa cha mwanadamu katika mwili mwengine huenda ukafanikiwa.

Madaktari watazindua mradi huo katika kongamano wakati wa msimu wa joto ,kwa lengo la kuanzisha utaratibu huo mnamo mwaka 2017.
Mtu atakayeongoza mpango huo ni daktari raia wa Italy Sergio Canavero kutoka kundi moja la wanasayansi mjini Turin.

Anaamini kwamba upandikishaji wa vichwa vya watu utawasaidia wanaosumbuliwa na magonjwa ya misuli na saratani.

Baada ya kutoa wazo hilo mnamo mwaka 2013,daktari Canavero anaamini vikwazo vikuu vya upasuaji huo vimekabiliwa ,kulingana na ripoti mpya ya wanasayansi.

Vikwazo hivyo ni pamoja na usimamizi wa uti wa mgongo kuingiliana na kichwa kipya pamoja na kuhakikisha kuwa kinga ya mwili haikikatai kiungo hicho kipya.
Daktari Canevaro alichapisha taarifa iliokuwa na nadharia kuhusu vile anavyoamini upasuaji huo unaweza kufanyika.

HIVI KU DU , KWICHI KWICHI KWENYE NDINGA NI KOSA LA KISHERIA AU KI MAADILI ????

  

BIASHARA ya kuuza miili imezidi kushamiri katika viunga vya Jiji la Mwanza na mwanzoni mwa wiki hii Kitengo Maalum cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers, kilifanya zoezi lingine kubwa baada ya kumnasa mwanamke mmoja akifanya mapenzi ndani ya gari katika eneo la Kirumba, Ijumaa lina data kamili.
Baada ya kutajiwa maeneo yanayosifika kwa biashara hiyo maarufu kama uchangudoa, OFM ambao juzikati walilifumua danguro lililopo maeneo ya Liberty jijini hapa, Jumanne wiki hii lilifanya matembezi katika eneo hilo ili kubaini jinsi biashara hiyo haramu inavyofanyika.

Majira ya saa tisa za usiku, katika eneo lililopo jirani na Villa Park, OFM ilishuhudia wanawake wengi wakiwa wamesimama na kujinadi kwa wanaume waliokuwa wakiwafuata na kuzungumza nao biashara kama wauzao vitu halali.

Baadhi ya waliokubaliana waliondoka kuelekea kusikojulikana na wengine, walisogea pembeni na ‘kujisevia’ kwenye maeneo ya giza.Lakini katika hali ya kushangaza, mwanamke mmoja akiwa na mwanaume, alionekana akiingia katika gari moja lililokuwa limeegeshwa katika eneo linalojulikana kama Magereji, lililopo pembeni ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa na OFM lilipowafuatilia, liliwabamba wakifanya mapenzi.

Wakati wakianza kupigwa picha mfululizo, mwanaume alifanikiwa kukimbia kwa kupitia dirishani na kutokomea bila kunaswa na kamera, wakati mwanamke alijikuta katika fedheha kubwa na kuanza kuomba msamaha kuwa picha yake isisambazwe kwa vile ataaibika.

Ijumaa: Sasa kwa nini unafanya biashara hii?
Mke wa mtu: Ni shida tu jamani, mume wangu kanitelekeza, naombeni mnisaidie msinitoe gazetini maana ndugu zangu wala hawajui kama nafanya biashara hii?

Baadaye katika uchunguzi wake, OFM ilibaini kuwa mlinzi wa gereji iliyopo eneo hilo ndiye amekuwa akitoa nafasi ya makahaba hao kutumia magari yanayolazwa eneo hilo kwa kuwatoza kiwango cha fedha ambacho hata hivyo hakikufahamika mara moja ni kiasi gani.

Hata hivyo, uchunguzi wa OFM umebaini kuwa machangudoa wengi wanaojiuza katika vijiwe vya Mwanza, wanatoza kati ya shilingi elfu nane hadi kumi kwa huduma ya muda mfupi, wakati wale wanaohitaji kulala nao, wanalipishwa kati ya shilingi 25,000 hadi 30,000.

Ijumaa linalaani biashara hii na linawatahadharisha wanaoifanya kuiacha la sivyo yatawakuta makubwa ikiwa ni pamoja na kuaibika kwa picha zao kuanikwa gazetini.

NILIKUA TAYARI KWA ADHABU YOYOTE .. KESI YANGU IMENIFUNZA MENGI .. CHIDI AKALISHWA

  

Rapper Chidi Benz kwa sasa ni mtu huru baada ya Alhamis hii kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi laki tisa. Amelipa faini hiyo.
Akizungumza leo kwenye ‘You Heard’ ya Clouds FM, Chidi amesema amejifunza mengi kupitia kesi hiyo.

“Nimejifunza kwa sababu kuna maisha halisi ambayo nimeishi kati hapo na matatizo. Ni maisha ambayo yamebadilisha sehemu kubwa sana ya maisha yangu,” amesema Chidi. “Kwanza watu wote wanafahamu tukio hili lilinitokea na nimemalizana nalo. Pia sijaisumbua mahakama, nilikubali kwamba ni kweli nimekutwa na hivyo vitu na ni kweli nilikutwa navyo na nikikataa ni sawa sawa na ujinga kwamba adhabu ni lazima nitapewa tu. Nilikuwa nipo tayari kwa adhabu yoyote,” ameongeza.

“Unajua mimi nimefanya tukio ambalo limeonekana ni tatizo kubwa sana kutokana na unajua sisi tunaishi na maadui kuna maadui wengine wanatengeneza suala lako kuonekana kubwa sana. Kwahiyo hakimu kaangalia huyu amekosea na amekubali anaweza akawa mfano kwa wengine. Kwahiyo watu wengine wajifunze na wajiweke sawa na wasafiri.”

Chidi amedai kuwa ni mama yake ndiye aliyeilipa faini hiyo.

“Mama yangu mzazi na rafiki yangu siwezi kumtaja, watu wawili tu ndo walikuwa pamoja na mimi. Mama yangu mzazi ameshughulikia kila kitu, faini pesa kulipa kila kitu kafanya yeye mama yangu mzazi. Kwahiyo mama yangu mzazi pekee ameshughulikia, namshukuru sana.”

IS YAWASHIKILIA MAMIA YA MATEKA SYRIA ..>>

     

Wanamgambo wa kundi la Dola la Kiislamu wameendesha mashambulizi dhidi ya vijiji kadhaa kaskazini mashariki mwa Syria, na kuwateka nyara mamia ya watu, zaidi ya 30 kuuawa na wengine kujeruhiwa.

Mamia kwa maelfu ya wakazi wa vijiji hivyo wamekimbilia katika miji mikuu ya mkoa, kama Hassaké au Qamichli.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, katika mij wa Istanbul, Jérôme Bastion, mapigano yamekua yakiendelea usiku wa Alhamisi Februari 26, kando ya mto Khabour ambako kunapatikana vijiji hivyo ambavyo vinakabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo wa kundi la wapiganaji wa Dola la Kislamu tangu Jumatau asubuhi wiki hii.

Kwa mujibu wa taarifa za mwisho tulizopokea kwa simu kutoka eneo hilo, hadi watu 350 wametekwa nyara katika vijiji hivyo. Inasadikiwa kuwa watu 110 miongoni mwa wanavijiji huenda waliuawa.

Kwa kweli inaaminika kuwa wanamgambo hao wa kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu waliwabeba wanawake na watoto katika mlima wa Abd al-Aziz, ulio karibu, ambao wameutenga kama ngome yao kuu.
Hata hivyo, wanamgambo hao wamewaacha vijijini wazee na wanaume kuwa kama ngao dhidi ya majeshi ya Kikurdi, na wapiganaji wa makundi mengine ambao wamekua wakijianda kujibu mashambulizi hayo.