Friday, 20 February 2015

YEMEN AIR KULIPAMAMILIONI KAMA FIDIA ...>>

 

Familia za wahanga wa ajali ya Yemenia Airways, iliyotokea tarehe 29 Juni mwaka 2009 katika pwani ya Moroni, zimefanikiwa...

Abiria 152 walifariki katika ajali hiyo, kijana mmoja pekee ndiye aliyenusurika kwa jumla ya abiria walikua ndani ya ndege hiyo.

Shirika la Yemenia Airways imetakiwa kulipa fidia ya Yuro milioni thelathini kwa ndugu 500 wa wahanga 70 miongoni mwa waliofariki katika ajali hiyo.

Kiwango hicho ni kidogo ikilinganishwa na Yuro milioni 70 iliyokua iliombwa na ndugu wa wahanga. Aidha, kesi 300 hazikuzingatiwa. Huu ni ushindi wa kwanza kwa familia za wahanga.

Kwa upande wa familia za wahanga, kwanza ni furaha baada ya miaka mitano ya mapambano mahakamani dhidi ya shirika la ndege la Yemenia Airways. Vita ambavyo familia za wahanga zimesema zilikua zilitelekezwa na shirika hilo la Yemenia Airways, baada ya shirika hilo kujaribu kukwepa wajibu wake baada ya ajali.

Baada ya uamzi wa Mahakama ya Aix-en-Provence, shirika la wahanga limesema kufurahishwa na uamzi huo, lakini limethibitisha kwmba litaendelea na kesi hiyo dhidi ya shirika la ndege la Yemenia Airways katika kitengo cha Mahakama kinachoshughulikia kesi za jinai.

No comments:

Post a Comment