4rm udaku..
KIMENUKA! Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE),
Ramadhan Kirungi amejikuta akiwa korokoroni ya Kituo cha Polisi cha
Daraja la Salenda jijini Dar baada ya kudaiwa ‘kufoji’ saini ya benki ya
wanachuo na kuchota shilingi milioni 31.
Kwa mujibu wa chanzo makini, wizi huo unadaiwa kubainika baada ya makamu
wake, Godfrey Modest kutumwa benki kwa ajili ya kutoa fedha ambazo
cheki yake ilishasainiwa.“Yule makamu aliporudi chuoni alimweleza
mhusika, akashagaa sana na hakuamini kilichotokea ndipo walipoamua
kumkamata rais huyo.
“Walipokwenda kumkagua kwake walimkuta na shilingi milioni 16.5 keshi
zilizosalia zikiwa zimefungwa katika mafungu matatu,” kilisema chanzo
chetu kikiomba hifadhi ya jina lake.
Baada ya habari hizo kutua kwenye Gazeti la Amani, mapaparazi wetu
walimtafuta msemaji wa chuo hicho, Leonidas Tibanga ambaye alikiri
kutokea kwa wizi huo na kuongeza kuwa hatua zimechukuliwa na mtuhumiwa
alikamatwa na kupelekwa polisi huku uchunguzi zaidi ukifanyika.“Ni kweli
wizo huo umetokea na hivi ninavyozungumza na wewe, mtuhumiwa yupo
polisi lakini uchunguzi zaidi unaendelea,” alisema Tibanga
No comments:
Post a Comment