Msanii nyota wa muziki wa Pop
Madonna alianguka katika jukwaa wakati alipokuwa akifanya shoo yake
katika tuzo kuu za muziki za Britts mwaka huu ,katika usiku ambao Sam
Smith na Ed Sheeran walishinda tuzo mbili kila mmoja .
Taylor Swift, alitajwa kama msanii mwanamke wa kimataifa wa kipekee. Katika sherehe hizo.
Madonna alijikwaa katika ngazi na kuaguka vibaya baada ya mchezaji densi mmoja kujaribu kutoa kofia aliokuwa amevaa mwanzoni mwa onyesho hilo.
Lakini hatahivyo mwanamuziki huyo alijikusanya na kuendelea kuimba wimbo wake Living for love.
Baadaye nyota huyo mwenye umri wa miaka 56 alitoa taarifa yake akisema kuwa yuko salama na kwamba kofia yake ilikuwa ikimbana sana.
''hakuna kinachoweza kunizuia na kwamba mapemzi yaliniinua juu''aliandika katika Istangram akinukuu maneneo katika wimbo wake.
No comments:
Post a Comment