Vikosi vya Jeshi la Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo FARDC, vimeanzisha hatua za kijeshi dhidi ya waasi
wa Rwanda wa kundi la FDLR, Jumanne hii .
Baadhi wa wajumbe wa kundi hilo wanashutumiwa kushiriki katika mauaji ya kimbari ya Rwanda kabla ya kutoroka katika nchi jirani ya Jammuhuri ya kidemokrasi ya Congo,ambako pia wanashutumiwa kutekeleza ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, yakiwemo mauaji, ubakaji na uporaji.
Mwandishi wa BBC wa mashariki mwa Kongo Byobe Malenga alituandalia taarifa ifuatayo.
Silaha nzito nzito pamoja na bunduki za rashasha zimesikika hii leo tangu asubuhi mapema katika vijiji vya Ruvuye na Mulindi katika misitu ya maeneo ya mji wa Lemera tarafani Uvira mkoani Kivu ya kusini .
Vyanzo vya idara ya 33 ya wanajeshi wa Mkoa zinaonyesha kuwa hatua hio nialama ya kuanza rasmi shughuli za kijeshi dhidi ya waasi hao wa kihutu toka Rwanda wa FDLR katika mkoa wa Kivu ya Kusini,huku vikisema kua askari wa taifa FARDC,wamedhibiti kambi ya Revo kutoka mikono mwa waasi hao kilomita thalathini na mji wa Lemera .
Kamanda wa harakati hizo maarufu "Sukola 2" dhidi ya wapiganaji wa Rwanda FDLR katika Kivu ya Kusini, Generali Esperant Masudi, yupo kwenye eneo la mapambano katika misitu ya Lemera ajili ya shughuli hizo.
Jeshi la Congo Kupitia Generali Didier Etumba, lilitangaza Januari 29 kama mwanzo wa operesheni dhidi ya waasi wa FDLR.
Lakini mapigano yalikuwa bado kuaanza katika maeneo yote ya hapa nchini.
Raia wa hapa mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo wameonyesha mtazamo wao kuhusiana na hatua hio ya jeshi la Congo FARDC kuanzisha mashambulizi dhidi ya waasi hao.
No comments:
Post a Comment