Inakadiriwa kuwa wachimbaji wapatao
mia tano wameokolewa na magari ya zima moto kutoka machimboni baada ya
kuwa wamebanwa chini ya mashimo yenye kina kirefu katika machimbo ya
madini nchini Afrika Kusini.
Mmiliki wa mgodi huo ni kampuni ya Harmony Gold wameeleza kuwa waliwaokowa wanaume zaidi ya mia nne na themanini na sita waliokuwa zamu siku hiyo .
Moto huo unasadikiwa ulianza wakati wa kazi ya matengenezo ilipokuwa ikiendelea.
Mwaka wa jana mgodi huo ulifungwa kwa muda wa wiki mbili ili kuwaondoa wachimbaji haramu ambao waliuvamia mgodi huo ambao wanshukiwa kuwa wao ndio walioanzisha moto huo.
No comments:
Post a Comment