Friday, 20 February 2015
UGANDA YAKUMBWA NA HOMA YA MATUMBO ...>>
Wizara ya afya nchini Uganda kupitia kwa mkuu wa huduma za afya nchini Uganda, Jane Ruth Achieng, amethibitisha kutokea kwa mlipuko wa homa ya matumbo katika mji mkuu wa Kampala na uchunguzi zaidi unafanyika.
Bi Achieng amewataka wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya homa ya matumba ambayo kwa kiasi kikubwa hutokana na kuwepo vimelea vya bakteria katika maji.
Maeneo yaliyoathirika mbali na Kampala, ni wilaya jirani za Mkono mashariki mwa mji wa Kampala na Wakisu iliyopo magharibi pamoja na maeneo ya Kusini na Kaskazini mwa mji wa Kampala.
Kugundulika kwa ugonjwa wa homa ya matumbo ni kufuatia uchunguzi wa kina uliofanyika baada ya kuwepo habari za kuzuka kwa ugonjwa wa ajabu uliowakumba watu kadha mji Kampala.
Kifo cha kwanza kutokana na ugonjwa huo kiliripotiwa Februari sita mwaka huu.
Dalili za ugonjwa huo ni homa, kusokotwa tumbo, maumivu ya viungo na kizunguzungu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment