Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama
ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC Fatou Bensouda amewasili
nchini Uganda ili kutafuta ushahidi kuhusu kesi ya aliyekuwa kamanda
mkuu wa wapiganaji wa LRA nchini Uganda .
Mwandishi wa BBC mjini Kamapala anasema kuwa Bensouda atazuru kazkazini mwa Uganda katika ziara ya siku tano ili kuzungumza na mashahidi mbali na kutembelea maeneo yaliotekelezewa uhalifu huo.
Pia anatarajiwa kukutana na rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa mahakama hiyo ya ICC akiishtumu kwa kuwabagua viongozi wa Afrika.
No comments:
Post a Comment