YAFANYWE YOOTE ... ILA KUMBUKENI TAIFA LINAWADAI .... WE HAVE THOUSANDS TO FEED THIS YEAR MNAJUA MVUA ZIMECHELEWA ?????? UNAJUA PESA IMEPOTEA MTAANI (KWENYE MZUNGUKO ) UNAJUA ZAIDI YA MILIONI 20 NI VIJANA AMBAO ZAIDI YA ASILIMIA 48 .. (48 %) HAWAJUI WATAKULA NINI THE NEXT MORN ... UNAWAJUA KINAMAMA WAGONGA KOKOTO , UMAWAJUA BODA BODA ??? ni hayo tu .. endelea
Dar es Salaam. Wakati Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka jana alitumia dakika 415 (takribani saa 7) akibishana katika mpambano mkali wa kisheria kuhusika kwake katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow, mwenzake wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge aliamua kutimkia Mahakama Kuu kukwepa kuhojiwa na Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Jana, mwenyekiti wa baraza hilo, Jaji Hamisi Msumi
alitoa uamuzi kuhusu pingamizi la Chenge aliyetaka baraza hilo
lisisikilize shtaka lake la kukiuka maadili ya uongozi wa umma.
Hata hivyo, Chenge alikwamisha kwa mara ya pili
baada ya kuomba kwenda Mahakama Kuu kutafuta tafsiri iwapo baraza hilo
linaweza kusikiliza shauri lake kinyume na amri ya mahakama iliyoagiza
lisijadilie na taasisi kwa kuwa kuna kesi kadhaa mahakamani
zinazohusiana nalo.
Profesa Tibaijuka na Chenge kila mmoja aliingiziwa
Sh1.6 bilioni kwenye akaunti zao binafsi kutoka kwa mkurugenzi wa VIP
Engineering iliyokuwa ikimiliki asilimia 30 ya hisa za kampuni ya
Independent Power Solution Limited (IPTL).
Baraza hilo, linasikiliza mashauri hayo kuhusu
ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka
1995 katika vipengele vya matumizi mabaya ya madaraka na sakata la
escrow.
Chenge, juzi katika baraza hilo alipoitwa kuhojiwa
aliibua hoja ya zuio la Mahakama Kuu na baada ya mabishano ya kisheria,
Jaji Msumi alisema angekwenda kuisoma amri huyo kisha kutoa uamuzi wake
jana.
Akisoma uamuzi huo, Jaji Msumi alisema:
“Mlalamikiwa ametoa hoja ya amri ya Mahakama Kuu kuwa ndiyo hiki
kinachojadiliwa, chimbuko lake ni miamala ya Akaunti ya Tegeta Escrow
ambalo chimbuko lake ni bungeni na mahakama ilizuia lakini amri hiyo
haizuii mamlaka hii.”
“Orodha ya taasisi zilizotajwa hailihusu baraza
hili, wadaiwa wote pamoja na mawakala, watumishi, wasaidizi wao au watu
wengine wanaofanya hili. Amri iliyoandikwa, Baraza si mlengwa wa hili.
Kinachozuiwa kufanywa ni kupelekwa bungeni au kujadiliwa taarifa ya
(Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali pamoja na umiliki wa
IPTL,” alisema.
Akihitimisha kusoma uamuzi wa baraza hilo, Jaji
Msumi alisema: “Hoja iliyotolewa na mlalamikiwa haina msingi na tunaomba
kuendelea kulisikiliza.”
Mara baada ya kumaliza, Chenge aliyekuwa amevalia
shati la kitenge na suruali nyeusi akiwa haonyeshi kuwa na wasiwasi
alisema: “Nashukuru kwa uamuzi huo lakini sina nia ya kubishana, natoa
hoja ya kukata rufaa ya kwenda Mahakama Kuu ili mahakama itafasiri kama
Baraza lina mamlaka ya kujadili suala hili.”
Chenge ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali alisema: “Kama wanasheria wa sekretarieti wangejituma kidogo
kwenda masijala ya Mahakama Kuu kupitia wangeliona hili. Amri hii ya
zuio ni pana kuliko uamuzi wa Baraza lako uliofikia, naomba nitumie
nafasi hii kwenda Mahakama Kuu.”
Akihitimisha hoja hiyo, Jaji Msumi alisema:
“Nakuruhusu, niongeze tu sina hakika kama kanuni zimetengenezwa kuruhusu
rufaa na kama hazipo kutakuwa na utaratibu. Ukipeleka itasaidia kujenga
Baraza lakini Mahakama Kuu ina haki, kila mtu ana haki kwa suala
lolote, mimi siwezi kukuzuia.”
No comments:
Post a Comment