Fainali za kombe la dunia kwa mwaka
2022 nchini Qatar huenda sasa zitafanyika mwezi Novemba au Decemba hiyo ni kwa
mujibu wa Mkuu wa kikosi kazi cha shirikisho la kandanda duniani Sheikh Salman
Bin Ebrahim amesema mapendekezo ilikuwa iwe mwezi May lakini wakati huo utakuwa
vigumu kwani ni majira ya fainali za michuano fainali za Klabu Bingwa barani
Ulaya.
Nchi ya Qatar imepewa jukumu la
kuandaa mashindano hayo mwaka 2022 lakini imegundulika kuwa fainali hizo
zitagongana na majira ya joto kali katika eneo hilo, jambo ambalo ni kikwazo wa
afya za wachezaji.
Mapendekezo mengine yalikuwa iwe
kati ya mwezi Januari au Februari lakini imeonekana zitagongana na mashindano
ya Olympic.
Hassan Al Thawad mkuu wa kamati ya
maandalizi ya finali hizo nchini Qatar ameiambia BBC kuwa Qatar imekubaliana na
mapendekezo ya kamati ya shirikisho la kanda nda duniani Fifa.
No comments:
Post a Comment