Wednesday, 25 February 2015

RIPOTI AMNESTY INTERNATIONAL YASEMA MAUAJI 214 NI AIBU ...>>

         
Ripoti ya Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International imesema jitihada za kimataifa za kila nchi kukabili vitendo vya mauaji ya halaiki yanayofanywa na makundi yenye silaha haziridhishi na ni aibu kwa dunia.

Katika ripoti mpya ya mwaka ya shirika hilo, makundi ya wanaharakati wa haki za binadamu wanauelezea mwaka uliopita wa 2014 kama mwaka wenye mauaji ya kutisha yanayofanywa na makundi hayo.
Ikiangalia mbali zaidi ya mwaka 2014 ripoti hiyo ya Amnesty international machafuko yaliendelea kulitesa bara la Afrika kwa takribani miaka 20 tangu kufanyika kwa mauaji ya kimbari ya Rwanda.

Machafuko mengine ambayo yanatajwa pia kusababisha mauaji makubwa ya halaiki ni mjibu wa Amnesty International ni yale ya Afrika ya Kati, Sudani Kusini, Somalia, Nigeria na Jamhuri ya demokrasia ya Congo.
Mivutano na mapigano yanasabaishwa na wapiganaji wenye silaha yanatajwa kusababisha hali isiyo ya kawaida ya mauaji pia na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kutokana na vitendo vyao.

Ripoti hiyo imesema kuwa makundi yaliyosahaulika katika jamii na ubaguzi vimeongeza kwa kiasi kikubwa ongezeko la machafuko na mivutano inayosababisha mapigano katika bara la Afrika.

Serikali za bara la Afrika zimelaumiwa ndani ya ripoti hii, kwa kile kinachotajwa kama matumizi mabaya ya majeshi dhidi ya raia katika mikusanyiko, mauaji hali kinyume na sheria pamoja na haki za binadamu.

Shirika hilo limesema kuwa kwa kipindi chote cha mwaka jana bara la Afrika lilijikuta likikumbwa na ongezeko la watu katika maeneo ya miji,ongezeko la maendeleo ya kiuchumi pamoja na kukumbwa na hali ya machafuko na mapigano,shughuli za kimaendeleo katika maeneo ya miji na hivyo kuongeza mbanano wa watu na shughuli za kiuchumi na kimaendeleo.

Nchi zilizo nyingi Afrika kwa mjibu wa Amnest International,kati hali hiyo ya kukumbwa na migogoro lakini bado zimeweza kuyafikia malengo ya millennia na kulifanya bara la afrika kuwa na nchi nane za juu kati ya kumi za mwanzo katika utekelezaji mzuri wa malengo ya millennia duniani.

Shirika hilo pia limesema kuwa umasikini barani Afrika bado ni tatizo kwa nchi nyingi,ambapo watu wake wanakabiliwa na umasikini japo kuwa wana laslimali nyingi asilia kama ilivyo kwa nchi za Nigeria Jamhuri ya demokrasia ya Congo.

No comments:

Post a Comment