Polisi wenye silaha na mabomu ya machozi pamoja na maofisa usalama, jana walitanda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kuzuia vijana waliopata mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wasimwone mwenyekiti wao, George Mgoba, aliyelazwa baada ya kutekwa na kuteswa na watu wasiojulikana.
Pamoja na hatua hiyo vijana wengine watatu akiwamo
katibu wa wahitimu hao walikamatwa na polisi na walikuwa wanashikiliwa
katika Kituo Kikuu jijini Dar es Salaam.
Mgoba Jumatatu iliyopita alitekwa, kuteswa na baadaye kutupwa kichakani katika eneo la Picha ya Ndege, Kibaha mkoani Pwani.
Kabla ya kufikishwa kwenye Hospitali ya Muhimbili,
Mgoba alilazwa kwenye hospitali ya Tumbi Kibaha na baadaye alihamishiwa
Hospitali ya Amana wilayani Ilala.
Jana, wahitimu hao wa JKT wanaokadiriwa kufikia
200 walifika katika lango la Hospitali ya Muhimbili saa 11.50 asubuhi na
kujichanganya na watu wengine waliokuwa wakisubiri kuwaona wagonjwa
wao.
Ilipofika saa 12.10 magari ya polisi matano kila
moja likiwa na askari sita yalifika katika eneo hilo na kuingia ndani ya
eneo la hospitali hiyo huku polisi waliovaa sare wakisimama kwenye
lango hilo kulinda usalama.
Makachero wengine waliingia ndani na kwenda moja kwa moja kwenye jengo la Mwaisela, wodi namba sita ambako Mgoba amelazwa.
Ilipofika saa 7.00 mchana watu waliofika kuangalia
wagonjwa waliruhusiwa kuingia ndani na baadhi ya wahitimu wachache
walijichanganya kwenda kuangalia wagonjwa.
Wengine wakamatwa
Hata hivyo, habari zilizopatikana baadaye na
kuthibitishwa na Kiwango zilisema kuwa aliyekamatwa ni katibu wa
wahitimu hao, Linus Emmanuel na wenzake wawili, ambao walitiwa mbaroni
wakati wakienda Muhimbili na wanashikiliwa katika Kituo Kikuu cha
Polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Mary Nzuki
hakupatikana kuthibitisha kukamatwa kwa vijana hao, lakini Kamanda wa
Kanda Maalumu ya Dar es Sa Salaam, Suleiman Kova alipoulizwa alisema
yeye yuko ofisini, vijana wake wanafanya kazi wakikamilisha wangempeleka
taarifa.
No comments:
Post a Comment