Man Man Man ... kuna
watu wako gizani ukifikiri wewe utoke vipi wengine waokolewe vipi vijana maaan
!
Huyu jamaa
alitelekezewa mtoto na demu wake , ambae nae ana miaka 17 sawa , jamaa hana
kazi , hana pa kulala , hana ndugu mjini na msela wake kamwondoa gheto
kwasababu sasa anamtoto na gheto kuna wahuni kama watano sita ambao wanakaa
kila siku achana na wakuja na kuondoka (vijana huwa hawakatazani kuja gheto ) ,
so jamaa analala na mtoto kwenye box barazani mwa gest kwa sasa .
Kwa machungu
yaliyotupata wa TUTOKE VIPI maisha yalete maana nikiwepo mie pia tuliamua
kuchangishana na ikapatikana kama 433,000/- pale pale kwanza tulipokua
tunaelimishana kuhusu maisha ya vijana na changamoto za vija nikiwa mwenyekiti
.
Na papo hapo
tukaamua kumnunulia sehemu ya chips na kumpa cash iliyobaki wakati anatafutiwa
pa kuishi na mdau JOSEPHAT N. MWAGESA aliyetokea kupenda na kuunga mkono
hii kazi yetu .
VIJANA MUNGU YUPO
TUTAFIKA ..
No comments:
Post a Comment