Monday, 23 February 2015

MAHAKAMA YAMSIKILIZA SIMONE GBAGBO KWA MARA YA KWANZA ..

         

Nchini Côte d'ivoire, sehemu ya kwanza ya kesi ya machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 na 2011, imemalizika Jumatatu wiki hii baada ya kusikilizwa Simone Gbagbo, mke wa aliye kuwa rais wa Côte d'ivoire, Laurent Gbagbo.

Machafuko hayo yaligharimu maisha ya watu 3000, huku watu 83 akiwemo Simone Gbagbo, wakituhumiwa kuhatarisha usalama wa taifa.

Simone Gbagbo alisikilizwa na Mahakama ya mjini Abidjan kwa muda wa saa 9. Kesi hiyo iligubikwa na mahojiano pamoja na ushahidi, ambapo Simone Gbagbo alikanusha tuhuma dhidi yake.

Jaji mkuu aliyefuatilia kesi hiyo, amezitaka pande zote husika katika kesi hiyo kukutana tena Jumatatu ya juma lijalo kwa kusikilizwa kwa mara ya mwisho.

Ni miaka minne sasa (tangu kukamatwa kwake), Simone Gbagbo alikuwa hajaonekana hadharani. Aliahidi kufanya hivyo kwa usalama wake.

Mmoja kati ya wanasheria wa Simone Gbagbo, Rodrigue Dadjé, amesema ameridhishwa na jinsi mteja wake alivyojieleza.

No comments:

Post a Comment