BY UDAKU BLG
Uteuzi wa Makonda ambao umefanywa na Rais Kikwete, unaonesha kuwashitua
wengi; hali ambayo imefanya watu wengi kumbeza hasa kupitia mitandao ya
kijamii.
Baadhi ya wanaobeza, wanadai kwamba Makonda hana sifa ya kuongoza wilaya
kubwa kama Kinondoni, ambayo ina changamoto na migogoro mingi ya ardhi.
Makonda ambaye ni Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji wa UVCCM, jina
lake limekuwa kubwa hivi karibuni baada ya kutuhumiwa kumpiga Jaji
Warioba wakati wa mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere.
Pia, kujitokeza kwake hadharani kumpinga Edward Lowassa, kuliongeza jina hilo kuwa maarufu.
Wakizungumza na Mpekuzi kwa nyakati tofauti, baadhi ya wasomaji wa
mtandao huu, wamedai kuwa uteuzi huo wa Rais ni mzuri ila alikosea
kumweka wilaya ya Kinondoni yenye matatizo chungu mzima ya kiutendaji
ikiwemo migogoro ya mipaka, ardhi, wafanyabiashara ndogondogo na mambo
mengine ya ndani.
“Tunampongeza Rais kwa kuteua wakuu wapya wa wilaya, ila kwa huyu Paul
Makonda kumweka Kinondoni, ameteleza. Hii wilaya inahitaji mtu mwenye
uzoefu mkubwa katika uongozi na uadilifu” alisema Sued Musa.
Naye Albert Chenza wa Dar alikuwa na haya ya kusema: "Ma-DC kama
Makonda wapo kwa ajili ya CCM kutetea maslahi ya CCM au wapo kwa ajili
ya wananchi kuwasaidia wananchi?
"Ikumbukwe DC ndiye Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya
na DSO akiwa katibu wake, sasa mtu kama Makonda ambaye yupo tayari
kufanya vurugu yoyote kutetea maslahi ya CCM leo kupewa u-DC wa
Kinondoni tutegemee nini uchaguzi mkuu wa Oct 2015?
"Ikitegemea kuna mvutano kati ya wapinzani na CCM ambao vyombo vya
usalama vinatakiwa kuleta haki na amani, wapinzani wategemee kupata haki
au NGUVU zao ndo itakuwa haki yao? Hakika nuru ya amani inafifia
Tanzania.
"Hii ni kama tupo disco la kukesha ambalo inatolewa CD hii inawekwa ile
na zote unahitaji unywe panadol kuzisikiliza." Alisema Albert na
kuongeza:
"Ni dhahiri sasa Mzee Warioba na Taasisi ya Mwalimu Nyerere wamemjua
adui yao halisi ni nani. Aliyekua mstari wa mbele kumshambulia na
kumfanyia fujo Mzee Warioba amepongezwa rasmi kwa kupewa ukuu wa
wilaya.
"Pia imeendelea kujidhihirisha sasa kuwa Ukitaka U-DC wewe mtukane
Lowassa kama Nape Nnauye, Mrisho Gambo na Makonda walivyofanya.
"Na pengine atakayekua jasiri vya kutosha na kumchapa angalao vibao viwili usoni anaweza kupata Ukuu wa Mkoa au Ubalozi kabisa"
Sailas Kassa Edward yeye anamaoni tofauti kidogo, na hapa anaanza
kwa kumpongeza Makonda: "Siku ya jana (juzi) Rais kikwete alifanya
uteuzi wa wakuu wa wilaya ambapo moja ya wateule ni paul Makonda.
"Inanishangaza sana kutoka jana(juzi) mpaka leo(jana) watanzania
wamekuwa wakilalamika kupitia mitandao ya kijamii wakikosoa uteuzi wa
ndgu makonda.
"Mimi binafsi nampongeza kwa nafasi aliyopata nadhani katiba ya jamhuri
ya muungano wa Tanzania haijampa rais mamlaka ya kuwatenga watu bali
kila mtu ana haki ya kuongoza na pia kuongozwa.
"Kwa watanzania itafika hatua kila mtu mwenye intrest za chama cha mapinduzi hamtaki apate nafasi je nani ana haki na nani hana?
"Nimejaribu kuchunguza haya yote yanatoka wapi mpaka makonda anakuwa
gumzo mtaani nikagundua kuwa wapenzi wa Edward Lowassa wameumia sana
kuona makonda anakuwa mkuu wa wilaya hasa ukizingatia anafichua mbinu na
hila za Lowassa na makundi yake. "
No comments:
Post a Comment