VITA ya kuwania kupitishwa na Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu sasa ni
kati ya Edward Lowassa na John Magufuli, Raia Mwema limeambiwa.
Wiki hii, gazeti hili limeambiwa kwamba Lowassa, waziri mkuu aliyejiuzulu, anatajwa kuungwa mkono na wajumbe takribani 220 wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), huku akiungwa mkono pia na zaidi ya nusu ya wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa chama utakaomchagua atakayekuwa mgombea wa chama hicho.
Magufuli anaelezwa kuwa kama ‘mgeni’ ndani ya chama lakini anatajwa kubebwa zaidi na rekodi yake ya utendaji ndani ya serikali; katika mwaka ambao Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kubebwa na ajenda kubwa ya uwajibikaji na ufisadi.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM ambaye amezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina, alisema kwa kadri anavyofahamu, vita sasa ni kati ya Lowassa na Magufuli ambaye ni Waziri wa Ujenzi.
“Nimefanya hesabu zangu na haya ndiyo majibu yake. Lowassa nafahamu tayari ana kura nyingi ndani ya NEC na Mkutano Mkuu. Nafahamu kwamba hivi tunavyozungumza ana takribani kura 220 kati ya takribani 300 za wa-NEC.
“Ana zaidi ya nusu ya kura zote za wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama. Sasa kama amenunua hao wajumbe au kawapataje hilo ni suala jingine. La msingi hapa ni kwamba kama uchaguzi ungefanyika leo ndani ya chama, Lowassa angeshinda,” alisema mjumbe huyo kutoka Tanzania Bara.
“ Kuhusu Magufuli, simuoni kama mtu mwenye nguvu ndani ya chama. Kwenye chama chetu kuna wanachama wa aina mbili; kuna wale tunaowaita Native CCM (CCM asilia) na Migrant CCM (Wahamiaji).
“Magufuli ni migrant. Hawa ni wale ambao wametumika zaidi serikalini kuliko kwenye chama. Hana ushawishi mkubwa miongoni mwa wajumbe wa NEC wala Mkutano Mkuu. Lakini usisahau, hata Benjamin Mkapa naye hakuwa asilia. Alikuwa mhamiaji lakini akawashinda wale asilia.
“Namna pekee ya wahamiaji kushinda ni endapo CCM itaamua kuwa na mgombea wa namna hiyo na hilo linawezekana kwa sababu limewahi kutokea huko nyuma.
“Huu ni uchaguzi ambao ajenda kubwa itakuwa ni uwajibikaji na ufisadi. Labda wote ni wawajibikaji wazuri. Lakini, CCM itakubali Lowassa apeperushe bendera ya kupinga ufisadi? Itakuwa inaonyesha picha gani kwenye vita dhidi ya ufisadi kwa kumpitisha Lowassa?” alisema mjumbe huyo ambaye kuna wakati alitajwa kuwa mmoja wa wanaotajwa kutaka kuwania urais.
Idadi hiyo ya wajumbe wa NEC wanaomuunga mkono Lowassa imetajwa kuwatisha wajumbe wa Kamati ya Maadili ya CCM ambao wanatarajiwa kukutana wakati wowote kujadili wanachama waliowekewa zuio la kufanya shughuli za kisiasa kwa mwaka mmoja.
Wiki iliyopita, kuliibuka taarifa ambazo hazijathibitishwa mpaka leo kwamba Lowassa ataongezewa adhabu kwa muda wa mwaka mmoja zaidi kwa madai kwamba alikiuka kifungo alichokuwa amepewa kwa kufanya shughuli za kisiasa.
“ Kuna taarifa kwamba wajumbe wa NEC wanaomuunga mkono Lowassa wanaweza kuamua kususia mkutano utakaotishwa kupitisha adhabu hiyo. NEC haiwezi kufikisha akidi kama wanaomuunga mkono Mbunge huyo wa Monduli hawatahudhuria. Hapo ndipo kazi ilipo,” alisema mmoja wa wajumbe wa NEC kutoka mkoa mmoja wa Kanda ya Ziwa.
Hata hivyo, mmoja wa wafuasi maarufu wa Lowassa, Mgana Msisindai, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, aliliambia gazeti hili kwamba uwezekano wa wajumbe kususia mkutano wa NEC ni mdogo.
“Mimi nafikiri haya mambo unataka kuyaleta mapema. Tusubiri kwanza tupate taarifa rasmi za chama kuhusu suala la wagombea waliowekewa zuio na halafu tuongee mambo mengine.
“Nikuhakikishie kwamba kuna mambo mazuri sana yanakuja. Wakati ukifika tutajua lakini suala la wajumbe kususia mkutano kama Lowassa ataadhibiwa sidhani kama lina ukweli. Wataingia tu wapambane humohumo,” alisema Msindai.
Katika mazungumzo hayo, Msindai alisema hafahamu kuhusu idadi ya wajumbe wa NEC au Mkutano Mkuu wa CCM wanaomuunga mkono Lowassa, lakini akaahidi kuwa hiyo ni taarifa ambayo inaweza kupatikana wakati mwafaka utapofika.
Lowassa na wana CCM wengine, Frederick Sumaye, January Makamba, Bernard Membe na William Ngeleja, walizuiwa kufanya shughuli zozote za chama kwa muda wa mwaka mmoja kwa madai ya kuanza kampeni kabla ya muda ulioruhusiwa na chama.
Katika toleo lililopita la gazeti hili, iliripotiwa kwamba ingawa hajazungumza hadharani na wala hatajwi kama mmoja wa wana CCM wanaopita kuomba waungwe mkono kwenye kinyang’anyiro hicho, Magufuli tayari amewaambia marafiki zake kwamba atajitosa.
Raia Mwema linafahamu kwamba Magufuli alimpa taarifa rafiki na swahiba wake kisiasa, Raila Odinga, aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Kenya, kuhusu uamuzi wake huo wakati alipokwenda kwenye msiba Januari mwaka huu.
Juhudi za kumpata Magufuli ili aeleze kuhusu dhamira yake hiyo hazikufanikiwa hadi tunakwenda mitamboni; na inaonekana wazi kwamba ameamua kufanya mambo yake kwa usiri mkubwa.
Namba yake ya simu ambayo imeandikwa kwenye kitabu cha namba za simu na mawasiliano na wabunge na mawaziri kilichotolewa na Bunge inapokewa na kijana mmoja ambaye alidai anaishi mjini Songea mkoani Ruvuma.
Juhudi za kupata namba ya simu ya Magufuli kupitia kwa mawaziri wenzake wanne ziligonga mwamba ambapo takribani wote walisema hawana namba yake ya simu.
Juhudi za kupata mawasiliano ya Magufuli kupitia kwa Waziri Kivuli wa Ujenzi, Felix Mkosamali, nazo ziligonga ukuta baada ya naye kusema hana mawasiliano ya waziri huyo zaidi ya yale yaliyo kwenye kitabu rasmi cha Bunge.
“Kusema kweli sina namba nyingine ya Magufuli kuliko ile ambayo inapatikana kwenye kitabu cha Bunge. Kama kwenye ile humpati basi inabidi umtafute msaidizi wake,” alisema mbunge huyo.
Raia Mwema lilifanya pia jitihada ya kuwasiliana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge, ambaye naye alidai hana namba ya bosi wake huyo na akaahidi kusaidia kumtafuta Magufuli lakini hakupatikana hadi tunakwenda hewani.
Mmoja wa watu wa karibu na Magufuli aliyezungumza na gazeti hilo kwa masharti ya kutotajwa jina alisema waziri huyo amegawa namba yake ya simu kwa watu wachache anaowaamini. - See more at: http://www.raiamwema.co.tz/ni-vita-ya-magufuli-na-lowassa#sthash.wO8T4wUS.dpuf
VITA
ya kuwania kupitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania urais katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu sasa ni kati ya Edward Lowassa na John
Magufuli, Raia Mwema limeambiwa.

No comments:
Post a Comment