Wednesday, 25 February 2015

SIASA MAREKANI ZATISHIA KUFUNGA SHUGHULI ZA SEREKALI ..>>

 Wananchi wakimsikiliza rasi Obama aliptangaza mabadiliko mkubwa ya Uhamiaji huko Hyattsville Md.

Mzozo mwingine wa kisiasa jijini Washington unatishia kufunga baadhi ya shughuli za serikali ya Marekani, wakati huu ukiwa juu ya fedha  fedha za kugharamia,  sera  inayopingwa ya rais Obama juu ya uhamiaji na wizara ya ulinzi wa ndani.

 Fedha zilizoidhinishwa awali katika bajeti ya matumizi ya serikali zitaisha Ijumaa  wiki hii, hali ambayo huenda ikapelekea  wafanyakazi 30,000  kubaki manyumbani na kuacha wengine laki 2 wakiendelea kufanya kazi bila malipo mpaka mzozo huo utafutiwe ufumbuzi.

Wabunge wa vyama vyote viwili, Republican na Demokrat, wanasema hawataidhinisha ombi la rais Obama la dola bilioni 40 katika mswada mpya wa matumizi ya fedha  za serikali kwa  ajili ya idara inayolinda mipaka ya nchi , wanaokagua viwanja vya ndege na walinzi wa rais Obama na familia yake.

 Chama cha upinzani cha Republican kinataka kuzuia mpango wa rais wa kuzuia  kufukuzwa Marekani wahamiaji takriban milioni tano wanaoishi  nchini kinyume cha sharia.

 Waziri wa wizara ya ulinzi wa ndani  ya Marekani Jeh Johnson amesema kwa jumla, ikiwa wizara yake itafungwa, kutakuwa na madhara makubwa  ikiwa ni pamoja  na kusindwa kwa wizara hiyo kulinda nchi.

No comments:

Post a Comment